Kocha
wa Manchester United, Louis Van Gaal amewalalamikia waandishi
wa habari kwa kuandika habari kuhusu yeye ambazo sio sahihi kuhusu
hatma yake ndani ya Manchester United kutokana na matokeo mabovu
wanayoyapata.
Van
Gaal aliingia katika mkutano na wanahabari na kuanza kuzungumza kuwa
wamekuwa wakiandika habari ambazo hazina ukweli ambazo zinakuwa
hazipendezi kwa kuandika kitu kisicho sahihi na kudanganya wasomaji
kuhusu hali halisi iliyopo.
“Mnatakiwa
kuwa na maelezo yenye usahihi, nilipokuwa nikipokea simu kutoka Ed
Woodward, Sir Alex Ferguson na David Gill sababu ya habari mnazoandika
zinakuwa siyo nzuri, hilo halina uhalisia na sasa natakiwa kujibu
maswali yenu lakini sidhani kama nahitaji kufanya hivyo”
Van
Gaal akaulizwa swali kuhusu kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kusema
maneno yanayosemwa kwa sasa kuhusu Van Gaal ni kumkosea heshima kocha
huyo na akajibu kwa kuuliza kama kuna mwandishi hajihisi kuwa na hatia
na anatakiwa kuomba msamaha kwake.
“Hakuna
mtu kwenye chumba hiki anahisi kuomba msamaha kwangu? Hilo
linanishangaza, ninafikiri kuwa nilifukuzwa, nililisoma hilo au
nilifukuzwa, au mwanafunzi wangu [Jose Mourinho] amechukua nafasi
yangu?,
“Mnafikiri
hili linamtokea mke wangu au watoto wangu? au wajukuu wangu? au
mashabiki wa Manchester United? au marafiki zangu? wananiita mara nyingi
tunazungumza na ndiyo maana Arsene Wenger kasema hivyo,” alisema Van
Gaal na kuongeza “Mnadhani nataka kuongea na vyombo vya habari kwa sasa?
nipo hapa sababu ya sheria za ligi ninatakiwa kuongea na nyie lakini
naona ninaloongea na nyie mnaliandika vile mnavyotaka nyie”
Baada
ya kuzungumza kuhusu kukerwa kwake na vyombo vya habari, akazungumzia
mchezo wao wa jumamosi siku ya kufungua zawadi “boxing day” dhidi ya
Stoke City na kusema “Hatupo katika nafasi nzuri kwa wiki nne
zilizopita, tulikuwa tukiongoza ligi na katika wiki nne mbele tunaweza
kuwa katika nafasi nzuri”
No comments:
Post a Comment