Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 2, 2013

NEWCASTLE YAIFUNGA CHELSEA 2-0, MOURINHO AKWAMIA ST. JAMES PARK, ANUNA NA KUPEWA KICHAPO CHA AIBU

Mchezaji wa Chelsea Kapteni John Terry kidogo aifunge Newcastle!!
Kikosi kilichoanza cha Chelsea.
Chelsea leo ikicheza Ugenini imenyukwa bao mbili na timu ya Newcastle walipocheza leo kwenye uwanja wao wa nyumbani. Mabao ya Newcastle yote yamefungwa kipindi cha pili katika dakika 68 kupitia mchezaji Yoan Gouffran baada ya kupigwa frii kiki na Yoan kujitisha kichwa safi na kufunga bao hilo mbele ya mabeki wa Chelsea. Bao la pili ni la jitihada baada ya Loïc Remy kufunga bao hilo dakika za majeruhi dakika ya 89 kwa kupewa pasi safi na kuachia shuti lililogonga mwamba na kuishilia kwenye lango la Chelsea.
Samuel Eto'o akililia kupewa penati baada mchezaji Yanga-Mbiwa kuonekana kama ameunawa na refa kuseha hakunaMchezaji Gouffran akishangilia bao lake kipindi cha pili.
Newcastle group celeb Gouffran
Wachezaji wa Newcastle wakishangilia bao kwa kupongezana kwa aina yake!!
Kocha wa Newcastle Alan Pardew akishangilia moja ya bao kwa timu yake kufunga
Torres kikabwa na mchezaji wa Newcastle Tiote na Ramires wakikimbilia mpira, Kipindi cha pili dakika ya 53 nafasi ya Tiote imechukuliwa na Anita baada ya Tiote kuondolewa.

No comments:

Post a Comment