Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 13, 2015

KUIONA YANGA NA PLATNUM 5000




KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Yanga SC na Platinum FC ya Zimbabwe kitakuwa na Sh. 5,000 kwa jukwaa la viti vya rangi bluu na kijani

Yanga wataikaribisha Platinum FC ya Zimbabwe katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, jumapili.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro alisema kwamba, katika jukwaa la viti vya Rangi Chungwa itakuwa Sh, 7000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000, na VIP A Sh 30,000.

Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumamosi Saa 2:00 asubuhi katika vituo vya Karume (Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom (Buguruni), BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).

Aidha, amesema magari yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya Uwanja siku hiyo.
Yanga SC imefika hatua hii baada ya kuitoa BDF XI ya Botswana, wakati Platinum iliing’oa Sofapaka ya Kenya.

Wakati huo huo: Kikosi cha Platinum kilichotarajiwa kuwasili Saa 2:00 usiku wa leo, hakijawasili na wenyeji wao, Yanga SC wameshangaa kwa sababu hawana taarifa nyingine.

“Sasa hatujui tunafanya nini, walituambia watafika Saa 2:00 usiku, lakini tumefika mapema sana kuwasubiri, hawajafika na hatuna taarifa nyingine,”amesema Muro.

Kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) timu mgeni itajigharimia gharama za malazi ugenini, lakini mwenyeji atawajibika kuwagharamia usafiri wa ndani.

No comments:

Post a Comment