MSHAMBULIAJI Mbaraka Yusuph ambaye msimu uliopita ameichezea Kagera Sugar na kufunga mabao 12 juzi alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Azam FC huku akizipiga chini ofa za Simba, Yanga na Singida United.
Juzi Jumatano mshambuliaji huyo alisaini mkataba wa awali wa makubaliano ya kujiunga na klabu hiyo huku akikubaliana na masharti yaliyomo kwenye mkataba huo.
Azam wamemaliza dili hilo na sasa mshambuliaji huyo ni mali yao halali kwa misimu hiyo miwili na atatambulishwa keshokutwa baada ya kumaliza majukumu yake na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ambayo ina mechi ya kufuzu Afcon dhidi ya Lesotho, itakayochezwa leo.
Azam walifanya mchakato wa usajili wa mchezaji huyo kwa siri kubwa na kwamba wameamua kusajili wachezaji wengi ambao ni vijana kwa lengo la kuwajenga zaidi kisoka.
Hivi
karibuni Azam pia ilimsainisha mshambuliaji wa Toto African, Waziri Junior
aliyemaliza mkataba na timu hiyo iliyoshuka daraja na bado wanaendelea kusajili
wachezaji wengine ambao wapo kwenye mipango yao ya muda mrefu
No comments:
Post a Comment