Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 25, 2014

EUROPA LEAGUE:ALHAMISI MECHI ZA LALA SALAMA RAUNDI YA MTOANO TIMU 32 KUPIGWA, SWANSEA CITY NA TOTTENHAM


FC Salzburg, ACF Fiorentina na Valencia CF wapo kwenye Nafasi nzuri sana za kusonga kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakati watakapocheza Mechi zao za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 Alhamisi Februari 27 huku wakiwa na ushindi mnono toka Mechi zao za kwanza.
FC Salzburg walipata ushindi mzuri Ugenini walipoichapa AFC Ajax Bao 3-0 na Valencia pia walishinda Ugenini Bao 2-0 walipoichapa FC Dynamo Kyiv, huku ACF Fiorentina watacheza kwao wakiwa na ushindi wa 3-1 dhidi ya Esbjerg fB.
Pia, Benfica na PFC Ludogorets Razgrad, watacheza Nyumbani kwao wakiwa wameshinda 1-0 katika Mechi za Ugenini.

Kwa Timu za Uingereza, Tottenham wako kwao White Hart Lane kurudiana na FC Dnipro Dnipropetrovsk wakiwa wamechapwa 1-0 huko Ukraine na Swansea City wanaenda huko Italy kurudiana na Napoli baada kutoka 0-0 huko Wales Wiki iliyopita.

EUROPA LIGI
RATIBA
Alhamisi Februari 27
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
20:00 FC Rubin Kazan- Russia v Real Betis-Spain [1-1]
21:00 Ludogorets Razgrad – Bulgaria v SS Lazio - Italy [1-0]
21:00 FC Basel 1893-Switzerland v Maccabi Tel-Aviv FC-Israel [0-0]
21:00 SSC Napoli - Italy v Swansea City AFC - Wales [0-0]
21:00 FC Shakhtar Donetsk -Ukraine v FC Viktoria Plzen - Czech Republic [1-1]
21:00 Eintracht Frankfurt - Germany v FC Porto – Portugal [2-2]
21:00 Sevilla FC - Spain v NK Maribor -Slovenia [2-2]
21:00 Red Bull Salzburg -Austria v Ajax Amsterdam – Netherlands [3-0]
23:05 KRC Genk -Belgium v FC Anzhi -Russia [0-0]
23:05 Tottenham Hotspur -England v FC Dnipro Dnipropetrovsk [0-1]
23:05 ACF Fiorentina - Italy v Esbjerg fB-Denmark [3-1]
23:05 Benfica - Portugal v PAOK FC – Greece [1-0]
23:05 Trabzonspor -Turkey v Juventus FC-Italy [0-2]
23:05 Olympique Lyonnais -France v Chernomorets Odessa-Ukraine [0-0]
23:05 AZ Alkmaar -Netherlands v Slovan Liberec - Czech Republic [1-0]
23:05 Valencia - Spain v FC Dinamo Kiev -Ukraine [2-0]

No comments:

Post a Comment