Timu ya CBE wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe |
Abukakar Amri (kulia) ambaye ni nahodha wa CBE akiwa aamini kuwa kombe wanalokabidhiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT) Dioniz Malinzi ni lao |
Liliana Meory (kulia) kwa upande wa mchezaji mmoja toka CBE akikabidhiwa kombe lake baada ya kuibuka bingwa kwa upande wa wanawake |
Sehemu ya umati uliofurika |
CBE wakiendelea na Mbwembwe zao |
Twanga pepeta wakitoa burudani |
CHUO Kikuu cha Biashara cha Dar es Salaam (CBE) leo kimetwaa ubingwa wa mashindano ya mchezo wa Pool Table kwa Vyuo Vikuu “Safari
Lager Higher Learning Pool
Championships” baada ya kukifunga Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tawi la Mbeya kwa
mabao 13 kwa 5 kwenye fainali zilizochezwa kwenye Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni.
CBE ambao walikuwa wanauwakilisha mkoa wa Dar es Salaam,
walikuwa na uchu wa kuchukua kombe kwani wamekuwa wakiishia nusu fainali kwa
miaka mitatu mfululizo.
Kwa matokeo hayo CBE walizawadiwa fedha taslimu 2,500,000 na
kombe, huku mshindi wa pili Chuo Kikuu cha Mzumbe akijichukulia 1,500,000.
Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Mzumbe ya Morogoro ambao pia
walipewa 1,000,000 na nafasi ya nne ilishikwa na Chuo Kikuu cha Mwanza, (SAUT)
na kupewa 500,0000
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja kwa wanawake nafasi ya
kwanza kwa Lilian Meory ambaye alipewa fedha taslimu 100,000 na ngao, nafasi ya
pili ilichukuliwa na Agness Jacob waChuo Kikuu cha SAUT ambaye alipewa 50,000.
Mchezaji mmoja mmoja kwa upande wa wanaume ilichukuliwa na
Said Mohamed wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO) na kupewa ngao pamoja na 150,000
huku George Tito wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro akiambulia 100,000.
Akizungumza kabla ya kutoa zawadi mgeni rasmi ambaye alikuwa
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Dioniz Malinzi, alipongeza
jitihada za bia ya Safari kwa kuanzisha mashindano hayo ambayo yameanza
kuiletea sifa Tanzania kimataifa na kukitaka Chama cha Mchezo wa Pool (TAPA)
kuendelea kushirikiana na bia ya Safari katika kuendeleza mchezo huo.
“Kwa kipindi kifupi nilichokaa hapa nimegundua kuwa
mashindano haya yameandaliwa vema na nampongeza meneja wa bia ya Safari, Oscar
Shelukindo kwa kazi nzuri kwani anekuwa hana mapenzi na michezo asingewekeza
kwenye pool table hivyo chama cha Pool mshikeni na mshirikiane nae vema”,
alisema Malinzi.
Pia bendi ya African Sttarw, wana kutwanga na kupepeta wametoa burudani safi kiasi cha kuwafanya mashabiki waliofurika Leader kuacha viti vyao na kuungana nao katika kusugua kisigino
Mashindano haya yalianza kutimua vumbi Mei 4, mwaka huu na yalishirikisha Vyuo Vikuu
vya mikoa ya Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza na
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment