USHINDI wa
timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars waliopata katika mchezo wa kufuzu
michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco umesaidia kuipandisha nchi
katika viwango vya ubora wa soka duniani.
Katika orodha hizo za kila mwezi
zilizotolewa leo Tanzania imekwea kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 119
waliyokuwepo mwezi uliopita mpaka nafasi ya 116 hivyo kuendelea kufanya vyema
ukilinganisha na mwaka jana.
Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Hispania
wameendelea kung’ang’ania kileleni mwa orodha hizo wakifuatiwa na Ujerumani
katika nafasi ya pili na Argentina katika nafasi ya tatu huku kwenye nafasi ya
nne kukiwa na ingizo jipya la nchi ya Croatia waliopanda wa nafasi tano mpaka
kufikia ya nne na tano bora inafungwa na Ureno.
Kwa upande wa Afrika,
Ivory Coast wameendelea kushika nafasi ya kwanza baada ya kupanda kwa nafasi
moja duniani mpaka nafasi ya 12 wakifuatiwa na Ghana katika nafasi ya pili
ambao wao wamedondoka kwa nafasi mbili mpaka ya 22 duniani. Mali wao wako
nafasi ya tatu wakifuatiwa na mabingwa soka barani Afrika Nigeria katika nafasi
ya nne na tano bora inafungwa na Algeria.
No comments:
Post a Comment