BAO pekee la Aaron Ramsey dakika ya 62, limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji Borussia Dortmund nchini Ujerumani.
Hilo linakuwa bao la 13 kwa mchezaji huyo msimu huu na bao la tano katika michuano ya Ulaya msimu huu. Pamoja na kufungwa, wenyeji ndio waliocheza vyema usiku huu na kabla ya Arsenal kupata bao lake, hawakuweza kutengeneza nafasi hata moja ya kufunga.
Borussia ambayo inapewa sifa ya moja ya timu bora kabisa Ulaya kwa sasa, iliingia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Stuttgart katika ligi ya kwao, Bundesliga, lakini ilikalishwa na mtutu mmoja wa bunduki.
Dortmund; Weidenfeller 6, Grosskreutz 7, Papastathopoulos 6, Subotic 7, Schmelzer 6, Sahin 5, Bender 5 (Hofmann 75, 5), Blaszczykowski 6 (Aubameyang 74, 5), Mkhitaryan 6, Reus 6 (Schieber 86), Lewandowski 6.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Arteta, Cazorla/Monreal dk75, Ozil, Rosicky/Vermaelen dk91 na Giroud/Bendtner dk90.
Ramsey akifunga bao muhimu
Dortmund ilipata nafasi nyingi nzuri ikapoteza
MECHI ZILIZOBAKI ZA ARSENAL:
Katika mechi nyingine, Barcelona imeifunga AC Milan mabao 3-1 Uwanja wa Camp Nou, Lionel Messi akifunga mawili dakika ya 30 na 83, wakati lingine limefungwa na Busquets dakika ya 40, huku Pique akijifunga dakika ya 45 kuwapatia wageni bao la kufutia machozi.
Barcelona: Valdes; Dani Alves, Pique, Mascherano, Adriano; Xavi/Song dk88, Busquets, Iniesta/Fabregas dk78, Alexis, Messi na Neymar/Pedro dk85)
AC Milan: Abbiati; Abate, Zapata, Mexes, Emanuelson; Muntari, Montolivo, De Jong, Poli/Birsa dk74', Kaka/Matri dk84, Robinho/Balotelli dk46.
Tano juu! Nyota wa Barcelona, Lionel Messi (kushoto) akishangilia bao lake la mwisho na mpishi wake, Cesc Fabregas
Kitu nyavuni! Messi akifunga bao la pili
Nayo Chelsea imeifumua 3-0 Schalke 04, mabao ya Samuel Eto'o dakika ya 31 na 54 na Demba Ba dakika ya 83.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Azpilicueta, Mikel, Cahill, Terry, Willian, Ramires, Eto'o/Ba dk77, Oscar/Lampard dk81 na Schürrle/De Bruyne dk78.
Schalke: Hildebrand, Uchida, Aogo, Neustädter, Höwedes, Matip, Draxler/Clemens dk62, Jones, Szalai, Boateng/Kolasinac dk77 na Fuchs/Meyer dk67.
Haraka mno: Samuel Eto'o aliuzuia mpira wa Timo Hildebrand kabla ya kuifungia Chelsea baola kwanza
Eto'o akimfuata kipa wa Schalke, Timo Hildebrand
Anauzuia: Eto'o aliunasa mpira na kuusukumia nyavuni
Eto's alifunga bao tamu sana
Eto'o akishangilia na kocha Jose Mourinho
Eto'o akifunga la pili
Willian akimpongeza Eto'o
Super sub: Demba Ba akifunga bao la tatu
Ba akishangilia bao lake
No comments:
Post a Comment