Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 26, 2015

KOCHA WA REAL MADRID CARLO ANCELOTTI AFUNGASHIWA VILAGO BAADA YA MIAKA 2


Carlo Ancelotti ametimuliwa kama Kocha wa Real Madrid baada ya kuiongoza kwa Misimu Miwili na kuiwezesha kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa mara ya 10.
Ancelotti, Raia wa Italy mwenye Miaka 55 ambae Mkataba wake na Real ulitakiwa kwisha mwishoni mwa Msimu ujao, Msimu uliopita alileta mafanikio Klabuni hapo kwa kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI na Copa del Rey na kisha kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Duniani lakini Msimu huu wametoka kapa bila Kombe.

Mafanikio pekee ya Real Msimu huu ni toka kwa Mchezaji wao Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, ya kutwaa Pichichi, Tuzo ya Mfungaji Bora La Liga huku Ubingwa wa Ligi hiyo ukienda kwa Mahasimu wao Barcelona.
Carlo Ancelotti ametimuliwa na Klabu ya  Real Madrid baada ya kutoka kapa.
Msimu huu, Real walishindwa kutetea Taji lao la UEFA CHAMPIONS LIGI baada ya kutolewa Nusu Fainali na Juventus ambao sasa watacheza Fainali na Barcelona hapo Juni 6.
Kwenye Copa del Rey walibwagwa nje na Atletico Madrid ambao nao walitupwa nje na Barca ambao Wikiendi hii watacheza Fainali na Athletic Bilbao.
Kwenye La Liga, Kikosi cha Ancelotti kimemaliza Nafasi ya Pili, Pointi 2 nyuma ya Mabingwa Barcelona.
Akitangaza uamuzi wa kumwondoa Carlo Ancelotti, Rais wa Real, Florentino Perez, alisema Jana: "Nini Ancelotti alikosea? Sijui. Ila Klabu hii inadai mambo makubwa. Mapenzi ya Wachezaji na Washabiki kwa Carlo ni makubwa kama vile kwangu kwake!"
Perez ameahidi kutangaza Kocha mpya Wiki ijayo huku Mhispania Rafael Benitez akitajwa sana kuwa mrithi.

Alipokutana na Uongozi wa Bodi ya Klabu ya Real Madrid  Ancelotti leo JumatatuRais wa Real Madrid Florentino Perez ameweka wazi kumtimua kocha wake  Ancelotti
Perez amekuwa akitimua timua Makocha ndani ya miaka  12kashatimu amakocha tisa

No comments:

Post a Comment