Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 24, 2017

MWAMUZI WA YANGA NA MAJIMAJI NA LIPULI NA MSHIKAMANO WAFUNGIWAMWAMUZI aliyechezesha mchezo wa Majimaji dhidi yaYanga Hussein Athuman ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wanaochezesha ligi kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Majimaji, Ruvuma.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Alfred Lucas alisema Athuman alipata alama za chini ambazo hazimwezeshi kuendelea tena kuchezesha ligi hiyo.
"Mwamuzi Athuman ameondolewa kwenye orodha na Yanga imetozwa faini ya milioni moja kwa kosa la kutoingia vyumbani pia kutumia mlango usio rasmi wakati wa kuingia uwanjani,"
Pia mwamuzi Ngole Mwangole amepewa barua ya onyo kali na kumtaka aongeze umakini wakati akichezesha mechi za Ligi Kuu baada ya kubainika kukataa bao lililoonekana kutokuwa na mushkeli la Mtibwa Sugar dhidi ya JKT Ruvu katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Naye mwamuzi Bryson Msuya amefungiwa mwaka mmoja kwa kutozingatia sheria ipasavyo wakati akitoa penalti dhidi ya timu ya Mshikamano FC, na ripoti yake kufanana na ile ya kamishna.
Pia mwamuzi msaidizi, Makongo Katuma amefutwa katika orodha ya waamuzi kwa kuwapiga vichwa wachezaji wawili wa Mshikamano FC na mwamuzi wa akiba, Hashim Mgimba ameondolewa kwenye ratiba kwa kuonyesha muda wa nyongeza tofauti na ule alioelekezwa na Mwamuzi.
Lucas alisema kamishna Fidelis Ndenga ameondolewa kwenye ratiba ya makamishna kwa taarifa yake kufanana na ya mwamuzi na kamishna Mnenge Seluja amepewa onyo kwa kosa la kutoripoti kitendo cha Pamba kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na wawakilishi watatu badala ya wanne.
Adhabu zote ni kwa mujibu wa kanuni za ligi zinazoendesha ligi husika.