Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 6, 2013

TAIFA STARS YATHIBITISHA KUWA HAIKUBAHATISHA KWA ZAMBIA, YAICHINJA CAMEROUN UWANJA WA TAIFA

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars wakimpongeza mfungaji wa bao pekee la Stars Mbwana Ally Samata alilofunga baada ya kupokea mpira wa krosi kutoka wingi ya kulia ya Frank Domayo zikiwa zimesalia dakika 3 mchezo kumalizika dhidi ya Cameroon. Mchezo huo umeafanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam jioni ya leo. Picha na Rahel Pallangyor.
Mwinyi Kazimoto ambaye leo hakuwa katika kiwango kizuri akijaribu kupiga shuti mbele ya nahodha wa Cameroon Pierre Wome Nlend. Mwinyi baadaye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Thomas Ulimwengu.
Kiungo Amri Kiemba ambaye yuko katika fomu hivi sasa akimtoka mlinzi wa kati wa Cameroon Ngoula katika mchezo uliochezwa hii leo uwanja wa Taifa.

Kocha wa zamani wa Simba Milovan Circovich naye alikuwepo uwanjani kushihudia mchezo huo. Habari zinasema kuwa kocha huyo yuko nchini kwa lengo la kufuatilia malipo ya kazi aliyoifanya klabu ya Simba.
Mshambuliaji wa TP Mazembe ya Congo na timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samata akimtoka mlinzi wa Cameroon Ngoula.
Kiungo mshambuliaji wa Taifa stars Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Cameroon

1 comment: