Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 16, 2013

DAVID BECKHAM KUSTAAFU SOKA MWISHONI MWA MSIMU HUU


David Beckham, Miaka 38, ametangaza kustaafu Soka mwishoni mwa Msimu huu baada ya kuwika katika Soka kwa Miaka 20, Beckham, Nahodha wa zamani wa England aliyoichezea mara 115, akiwa na Mabingwa wa England, Manchester United, aliweza kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 6 pamoja na UEFA CHAMPIONZ LIGI. 

Mwezi Januari, Beckham alisaini Mkataba wa kuichezea Paris St-Germain ya France kwa Miezi mitano.
PSG wamebakiza Mechi 2 Msimu huu, ile ya Nyumbani dhidi ya Brest Jumamosi hii na Ugenini na Lorient hapo Mei 26.

Beckham alishinda tuzo iliyotolewa na BBC 2010

Beckham pia alishinda MLS na kuwa juu huko Los Angeles Galaxy
Beckham akiteta na Gary Neville, kwenye ligi wakati waliposhinda mataji yote mwaka 1999 wakati huo akiwa Manchester United.

Beckham pamoja na kuamua kustaafu amestaafu akiwa bado yupo safi kisoka japo umri kuonekana kusonga mbele akiwa na miaka 38 hivi sasa.

Enzi hizo Beckham akiwa amepiga magoti chini kushoto timu Ridgeway Rovers
Beck akiwa kitaa cha Waltham Forest mwaka 1989 akiwa na miaka 14 tu

Miaka 10 iliyopita akiwa na Nelson Mandela Africa kusini
Beckham akisalimiana na Mbrazil Pele kwenye eneo la gala New York mwaka 2008
Beckham na Muhammad Ali huko London mwaka uliopita

Rais Barack Obamba akimkaribisha White House kipindi cha nyuma kidogo kwenye wito wa maalum wa LA Galaxy
Beckham, ambaye Mshahara wake akiwa na PSG huenda kwenye Mifuko ya Hisani ya kusaidiaWatoto, ameichezea PSG Mechi 13 tangu ahamie hapo.
Akiwa na Klabu za Man United, Real Madrid, Los Angeles Galaxy, AC Milan na PSG, amefanikiwa kutwaa Makombe 19 na Ubingwa wa Ligi za Nchi mara 10.

Beckham ametamka: “Ungeniambia nilipokuwa Mtoto kuwa ningechezea na kutwaa Mataji na Klabu niliyoipenda ya Manchested United, kuwa Nahodha wa Nchi yangu kwa fahari kubwa na kuichezea zaidi ya mara 100 na kuzichezea Klabu kubwa Duniani, ningekwambia hiyo ni ndoto!”
Aliongeza: “Nimebahatika kutimiza Ndoto hiyo!”
Beckham, aliezaliwa Mei 2, 1975, alijiunga na Man United Mwaka 1991 akiwa Mcheza Soka Mwanafunzi na kuanza kuichezea Timu ya Kwanza Mwaka 1992 na kusaini Mkataba wake wa kwanza wa Mchezaji wa Kulipwa Mwaka 1993.

Akiwa Old Trafford, Beckham alijijengea Jina kubwa Duniani kote na umaarufu wake kuongezeka pale alipomuoa Mwimbaji maarufu wa Kundi la Spice Girls, Victoria Adams.
Mwaka 2003 Beckham aliihama Man United na kwenda Spain kuichezea Real Madrid ambako alifanikiwa kutwaa Taji la La Liga Mwaka 2007 na kisha kuhamia Marekani kuichezea LA Galaxy.

Akiwa na LA Galaxy, mara mbili, Mwaka 2009 na 2010, Beckham alicheza kwa Mkopo huko Italy na Klabu ya AC Milan.

KUHUSU DAVID BECKHAM
Manchester United
Premier League – 1996, 1997, 1999, 200, 2001, 2003
Champions League – 1999
FA Cup - 1996, 1999
Community Shield – 1993, 1994, 1996, 1997
Intercontinental Cup – 1999
FA Youth Cup – 1992
Real Madrid
La Liga - 2007
Spanish Super Cup – 2003
LA Galaxy
MLS Cup – 2011, 2012
Paris Saint-Germain
Ligue 1 - 2013   

No comments:

Post a Comment