Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars wakimpongeza mfungaji wa bao pekee la Stars Mbwana Ally Samata alilofunga baada ya kupokea mpira wa krosi kutoka wingi ya kulia ya Frank Domayo zikiwa zimesalia dakika 3 mchezo kumalizika dhidi ya Cameroon. Mchezo huo umeafanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam jioni ya leo. Picha na Rahel Pallangyor. |
Mwinyi Kazimoto ambaye leo hakuwa katika kiwango kizuri akijaribu kupiga shuti mbele ya nahodha wa Cameroon Pierre Wome Nlend. Mwinyi baadaye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Thomas Ulimwengu. |
Kiungo Amri Kiemba ambaye yuko katika fomu hivi sasa akimtoka mlinzi wa kati wa Cameroon Ngoula katika mchezo uliochezwa hii leo uwanja wa Taifa. |
Mshambuliaji wa TP Mazembe ya Congo na timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samata akimtoka mlinzi wa Cameroon Ngoula. |
Kiungo mshambuliaji wa Taifa stars Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Cameroon |
Safi sana hii
ReplyDelete