Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 3, 2017

SERENGETI BOYS UWANJANI LEO NA CAMEROON
TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17,’ Serengeti Boys’ leo inashuka tena uwanjani kucheza na Cameroon mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
 Serengeti boys inarudiana tena Cameroon baada ya juzi kuifunga bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Ahmadou Ahijo, mjini Yaounde.
Akizungumza na gazeti hili, kocha Mkuu wa Serengeti boys, Bakari Shime alisema kikosi chake kinazidi kuimarika siku hadi siku na wapo tayari kwa ushindi mwingine .
“Leo tunarudiana na Cameroon, vijana wana ari ya kuifunga tena Cameroon kwenye ardhi yao, cha msingi naomba watanzania wazidi kuwaombea vijana wao ili wawe na afya njema,” alisema Shime.
Katika mchezo wa juzi ambao ulihudhuriwa na gwiji wa soka barani Afrika Rogger Milla , bao pekee la Serengeti Boys lilifungwa na Ally Ng'anzi dakika ya 36.
Serengeti Boys ilitua Younde, Cameroon wiki iliyopita kitokea Morocco ambako iliweka kambi na kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Gabon na kushinda 2-1 kila mchezo.
Serengeti Boys imeshacheza mechi tano tangu kuanza kambi ya maandalizi ya fainali za Gabon, baada ya awali kuifunga Burundi mara mbili, Machi 30 mabao 3-0 na Aprili 1 mabao 2-0, mechi ambazo zilichezwa Uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Ikiwa nyumbani Serengeti boys ilicheza na Ghana ‘Black Starlets’ Aprili 3  katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kulazimishwa sare ya mabao  2-2
Mei 7 Serengeti boys inarajiwa kuwasili Gabon ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola na Cameroon nayo itashiriki fainali hizo ikiwa imepangwa kundi A lenye timu za wenyeji, Gabon, Guinea na Ghana.