Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 7, 2015

DAKTARI MWANAMKE, EVA CARNEIRO WA CHELSEA AKEJELIWA NA MASHABIKI

TUHUMA nzito zimeibuka huko Uingereza kwamba Mashabiki wa Timu pinzani mara nyingi huimba maneno ya kashfa ya kumdhalilisha kijinsia Daktari Mkuu wa Chelsea, Eva Carneiro, ambae ni Mwanamama.
Tuhuma hizi zimeibuliwa na uchunguzi wa Video za BBC, Shirika la Utangazaji la Uingerea, pamoja na Mitandao mbalimbali ambayo pia imenukuliwa kumshambulia Refa Msaidizi, Mshika Kibendera Mwanamama, Helen Byrne.

Matukio hayo yameifanya FA, Chama cha Soka England, kuwahimiza Mashabiki wa Soka kutoa Ripoti za Mashambulizi ya Ubaguzi wa Kijinsia huku Klabu ya Chelsea ikitaka Watu kuacha kashfa hizi za kishenzi.
Msemaji wa Klabu ya Chelsea amesema: “Suala la Usawa wa Kijinsia tunalichukulia kwa uzito mkubwa na tunashutuma sana ubaguzi wa aina yeyote ukiwa pamoja na wa Jinsia!”Shutuma hizi zimeibuka baada ya Utafiti toka Chombo cha Kupinga Ubaguzi kwenye Soka, Kick It Out, kutoboa Matukio 13 ya Ubaguzi wa Kijinsia kwenye Viwanja vya Soka vya Kulipwa na vinginevyo kwa Kipindi cha Agosti hadi Desemba 2014.

No comments:

Post a Comment