Samia awakumbusha wajibu Polisi, akiomboleza vifo vya watu 21
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, kufuatia vifo vya watu 21 vilivyotokana na ajali ya barabarani iliyotokea mkoani humo tarehe 09 Novemba, 2026.
Katika taarifa hiyo, Rais Dkt. Samia ametoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, ndugu, jamaa, na marafiki, na kuwaombea nguvu, subira na faraja katika kipindi hiki cha majonzi, huku akiwatakia majeruhi wote uponyaji wa haraka.
Aidha, amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia sheria za usalama barabarani, na kuwasihi madereva na watumiaji wote wa barabara kuchukua tahadhari na kuzingatia sheria ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, alieleza kuwa ajali hiyo ilitokea katika eneo la Njiapanda ya Kiponzero, ikihusisha basi la abiria na lori la mizigo. Katika ajali hiyo, ya uso kwa uso watu 21 walipoteza maisha papo hapo au kutokana na majeraha makubwa, huku watu wengine watano wakikimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.



Post a Comment