KAMATI YA URATIBU YA KITAIFA YA WATAALAMU WA MAANDALIZI YA AFCON 2027 YAPITIA TAARIFA ZA KAMATI NDOGO
Kamati ya Uratibu ya Kitaifa ya Wataalamu wa Maandalizi ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) imekutana leo, Novemba 6, 2026, kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Kamati Ndogo mbalimbali zinazohusika na maandalizi ya michuano hiyo.
Katika kikao hicho, taarifa zilizowasilishwa zimehusu maeneo muhimu ya maandalizi, ikiwemo Miundombinu, Ulinzi na Usalama, Usafirishaji pamoja na Fursa za Kiuchumi, ambapo wajumbe wamejadili hatua zilizofikiwa, changamoto zilizopo na masuala mbalimbali yanayohitaji kupewa kipaumbele ili kuhakikisha maandalizi yanaendelea kwa kuzingatia mahitaji na viwango vya michuano hiyo.
Aidha, kikao hicho kimejadili mikakati ya kuimarisha uratibu na ushirikiano baina ya wadau mbalimbali ili kuhakikisha maeneo yote muhimu yanakuwa katika hali ya utayari kuelekea AFCON 2027.
Kesho, Novemba 7, 2026, Kamati hiyo inatarajiwa kufanya ziara ya kukagua hali ya utayari wa miundombinu na maeneo mbalimbali ya maandalizi ya AFCON 2027 jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo inalenga kujionea maendeleo ya maandalizi katika maeneo husika na kubaini hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha Tanzania inakuwa tayari kushiriki katika maandalizi ya pamoja ya kuandaa michuano hiyo kwa mafanikio.
AFCON 2027 inaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.
Post a Comment