Tuzo za Cheza kidansi Desemba 9
TUZO pekee za muziki wa dansi Afrika Mashariki, Cheza Kidansi zikiwa katika msimu wa tisa mfululizo zitatolewa Desemba 9, mwaka huu mkoani Dar es Salaam.
Tuzo hizi ambazo zimekuwa chachu ya utoaji wa kazi nyingi za dansi, ushindani, ubunifu, ubora, hamasa ya dansi, ajira na kukuza sanaa nchini, zitakwenda sambamba na sherehe za miaka 15 ya Cheza Kidansi.
Akizungumza mratibu wa tuzo hizo, Bernard James alisema siku hiyo matukio mbalimbali yatafanyika ikiwa ni pamoja na kuwakumbuka na kuwatambua nguli wa muziki wa dansi waliosahaulika.
Alisema utoaji wa tuzo hizo utasindikizwa na burudani ya muziki wa dansi kutoka kwa bendi zilizosheheni mastaa wa muziki huo nchini.
Aliwaomba wadau kujitokeza kudhamini tukio hilo muhimu lililo kwenye kalenda ya muziki wa dansi nchini. Cheza Kidansi iliasisiwa mwaka 2011, ikiwa kinara wa kuutangaza muziki wa dansi nchini.
Post a Comment