Serikali yaaga waogeleaji 45
WAOGELEAJI 45 wameagwa na serikali kwa ajili ya kwenda kwenye mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika yanayofanyika Kampala nchini Uganda.
Akizungumza wakati wa kuwaaga waogeleaji hao Dar es Salaam jana, Ofisa Michezo Mwandamizi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Charles Maguzu aliwataka kutumia mashindano hayo yatakayoanza leo na kumalizika Oktoba 25, mwaka huu kutumia kupima uwezo wao dhidi ya washindani kutoka mataifa mengine na kuonesha matokeo ya maandalizi waliyofanya.
“Tunawaomba waogeleaji wetu mkapambane kwa nguvu zote ili kuhakikisha tunatwaa ubingwa huo,” alieleza Maguzu. “Tunaamini wana uwezo wa kufanya vizuri na kulitangaza taifa letu kupitia mchezo wa kuogelea,” aliongeza.
Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha waogeleaji kutoka mataifa mbalimbali ya Kanda ya Tatu Afrika, yakiwa fursa kwa Tanzania kupima uwezo wa wanamichezo wake katika makundi mbalimbali ya umri na kuimarisha ushindani katika mchezo wa kuogelea.

Post a Comment