RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WAPYA WA TTB NA TBA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbili za serikali kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.
Katika uteuzi huo, Dkt. Thereza Israel Mugobi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), nafasi ambayo alikuwa akiikaimu kabla ya uteuzi huo rasmi.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais amemteua Bw. Said Rajabu Mndeme kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), akichukua nafasi ya Bw. Daud Kondoro ambaye amemaliza muda wake wa utumishi.
Kabla ya uteuzi huu mpya, Bw. Said Rajabu Mndeme alikuwa akihudumu kama Mkurugenzi wa Milki katika Wakala huo wa Majengo Tanzania (TBA).

Post a Comment