RAIS SAMIA AMPOKEA RAIS WA ANGOLA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 29 Oktoba, 2026 amempokea rasmi Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço, ambaye yuko nchini kwa Ziara ya Kitaifa katika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Sherehe za mapokezi zilianza mara baada ya kiongozi hقي huyo wa Angola kuwasili katika viwanja vya Ikulu, ambapo alisalimiana na mwenyeji wake Dkt. Samia Suluhu Hassan kabla ya kusimama pamoja kupokea heshima ya Nyimbo za Taifa za Tanzania na Angola. Baadaye, Rais Lourenço alilikagua Gwaride Rasmi la Mapokezi lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mapokezi hayo yaliyopambwa na matukio mbalimbali yalihudhuriwa pia na viongozi na wananchi, huku viongozi hao wawili wakipata fursa ya kuangalia vikundi vya ngoma za asili. Kabla ya kuanza kwa mazungumzo rasmi, Rais Lourenço alisaini Kitabu cha Wageni katika ukumbi wa Ikulu.
Baada ya sherehe za mapokezi na tukio la kusaini kitabu cha wageni, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo Ujumbe wa Angola uliongozwa na mgeni wake huyo, Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço, kwa lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria na kiuchumi kati ya nchi hizi mbili wanachama wa SADC.
Wakatiu huo huo Rais huyo wa Angola, anatarajiwa kuungana na Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa Mji wa Kiserikali wa Mtumba, Dodoma kesho.
Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali imeeleza ziara hiyo iliyoanza jana inalenga kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Angola, kufungua fursa mpya za ushirikiano na kusisitiza dhamira ya nchi hizo katika kuhimiza amani, usalama na utangamano wa kikanda.
Mji wa Kiserikali wa Mtumba mkoani Dodoma ni mradi unaolenga kuunganisha taasisi za serikali, kuimarisha uratibu na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.
Rais Lourenço alipokelewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo.
Ziara hiyo ni ya kwanza tangu aliyekuwa Rais wa kwanza, Dk António Neto alipotembelea Tanzania mwaka 1979. Ziara hiyo ni mwendelezo wa uhusiano wa muda mrefu na undugu kati ya Tanzania na Angola, uliojengwa katika misingi ya mshikamano na ushirikiano wa ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.
Kupitia ziara hiyo nchi hizo zinatarajia kuendeleza urithi huo wa kihistoria, kuimarisha ushirikiano wa uwili na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kwa manufaa ya nchi zoteKatika sekta ya uchumi na biashara, Angola inajivunia kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi imara na fursa nyingi barani Afrika, huku uti wa mgongo wa uchumi wake ukitegemea sekta ya mafuta ghafi na gesi asilia ambapo inashindana katika nafasi za juu za uzalishaji barani humu.
Pamoja na nishati, nchi hiyo inatambulika duniani kote kwa uzalishaji wa almasi yenye thamani kubwa na akiba ya madini mengine kama chuma, shaba na dhahabu.
Pia, uwepo wa ardhi yenye rutuba na vyanzo vingi vya maji unaipa uwezo mkubwa wa kilimo na uzalishaji wa nishati ya maji, huku ikitawala lango la biashara ya kimataifa kuelekea mabara ya Amerika na Ulaya kupitia bandari zake za kimkakati katika Bahari ya Atlantiki kama vile Luanda, Lobito na Namibe.
Licha ya jiografia kuweka umbali mkubwa kati ya Tanzania iliyopo Pwani ya Bahari ya Hindi na Angola iliyopo Pwani ya Atlantiki, nchi hizi mbili ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zina fursa kubwa za kufaidishana kiuchumi.
Tanzania inaweza kufaidika kwa kujifunza uzoefu wa kiteknolojia na usimamizi wa mikataba ya mafuta na gesi (LNG) kutoka Angola, pamoja na ushirikiano katika uchimbaji na usindikaji wa madini. Zaidi ya hayo, kupitia Ukanda wa Usafirishaji wa Lobito (Lobito Corridor), Tanzania ina fursa ya kuunganisha mifumo yake ya usafirishaji kama TAZARA na Bandari ya Dar es Salaam ili kutengeneza njia kuu ya kibiashara inayovuka bara zima kutoka Bahari ya Hindi hadi Atlantiki.
Katika sekta ya biashara na huduma, Tanzania ina fursa kubwa ya kutumia tegemeo la Angola la kuagiza chakula kutoka nje kwa kuuza bidhaa za nafaka kama vile mahindi, mchele, maharage na mazao mengine ya kilimo.
Ushirikiano huu unaweza kuimarishwa zaidi kupitia usafiri wa anga kati ya mashirika ya ndege ya nchi hizi mbili, hatua inayotarajiwa kurahisisha mwingiliano wa watalii, wafanyabiashara na kuimarisha diplomasia ya kiuchumi kati ya ukanda wa Afrika Mashariki na ule wa Atlantiki.

















Post a Comment