RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI WA BODI TAWA, TTB NA TANAPA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za taasisi mbalimbali za serikali za mali asili ,utalii na uhifadhi nchini. 

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, katika uteuzi huo, Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA). 

Eneo lingine lililoguswa na uteuzi huo ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), ambapo Bi. Zuhura Sinare Muro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo. Uteuzi wake unatarajiwa kuongeza chachu katika kuhamasisha na kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

Pia, Rais Samia amemteua Meja Jenerali Mstaafu Hamis Rajab Semfuko kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA). 

No comments