HISTORIA YA KUSISIMUA YA ‘GANGSTER GRANNY’: BIBI WA MIAKA 100 ANAYEMZIMIA MESSI
Pauline Kana, anayefahamika duniani kote kama 'Gangster Granny', ni bibi
wa miaka 100 kutoka nchini Marekani ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kupitia
video za ucheshi anazozitengeneza akishirikiana na mjukuu wake, Ross Smith.
Mbali na umaarufu wake kwenye
mitandao ya kijamii, Pauline amevutia hisia za watu wengi duniani kutokana na
mapenzi yake makubwa na ya dhati kwa nahodha wa timu ya taifa ya Argentina,
Lionel Messi.
Bibi huyu ameandika historia ya kipekee kwa kuwa mmoja wa watu wachache
waliojaliwa kuishi na kushuhudia mashindano yote ya Kombe la Dunia tangu toleo
la kwanza lililofanyika mwaka 1930 hadi lile la mwaka 2026.
Katika mashindano ya mwaka huu, alionekana mara kadhaa viwanjani akiwa
amevalia jezi ya Argentina na kubeba mabango yaliyoonyesha wazi mapenzi yake
makubwa kwa Messi, kitendo kilichowagusa na kuwafurahisha mashabiki wengi wa
soka duniani.
Kama ishara ya upendo na kuthamini uaminifu wake wa muda mrefu kwa
mchezo wa soka pamoja na mapenzi yake kwa nyota huyo, Lionel Messi aliamua
kumzawadia jezi yake rasmi.
Tukio hilo la kupokea zawadi hiyo lilimletea Pauline furaha kubwa na
kuwa moja ya matukio yaliyogusa hisia za mamilioni ya mashabiki, huku
likionyesha heshima ya juu aliyonayo Messi kwa bibi huyo ambaye ameshuhudia
historia nzima ya Kombe la Dunia katika kipindi chake cha kuishi.

Post a Comment