REFA ALIYEZUILIWA KUINGIA MAREKANI APOKELEWA KISHUJAA
Mwamuzi wa kimataifa kutoka Somalia, Omar Artan,amepokelewa kwa shangwe katika Jiji la Mogadishu baada ya kukosa visa ya kuingia Marekani ambako alikuwa amepewa jukumu la kushiriki katika Kombe la Dunia 2026.Artan amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde na kupokewa na umati mkubwa wa wananchi pamoja na viongozi wa serikali waliokuwa wamejitokeza kumpokea.
Mwamuzi huyo alikuwa miongoni mwa walioteuliwa na FIFA kushiriki Kombe la Dunia la FIFA 2026, lakini alikwama kusafiri baada ya kushindwa kupata kibali cha visa akiwa nchini Morocco.
Kwa mujibu wa taarifa za FIFA, Artan alizuiwa kuingia Marekani baada ya kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami, lakini amamlaka za uhamiaji nchini humo hazijatoa sababu rasmi ya hatua hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa Somalia ni miongoni mwa nchi zilizo kwenye orodha ya vikwazo vya usafiri vilivyoanzishwa na utawala wa Marekani, jambo linaloendelea kuibua mjadala kimataifa kuhusu vikwazo vya usafiri kwa watendaji wa michezo.
.webp)
Post a Comment