JITAYARISHENI KWA EL NINO



Wanasayansi wana hofu kuwa athari za pamoja za El Niño na mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu zinaweza kubadili hali ya hewa duniani.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa awamu mpya ya hali ya hewa ya asili ya El Niño inaweza kuanza ndani ya wiki chache, hatua inayotarajiwa kuongeza joto duniani katika kipindi ambacho tayari sayari iko chini ya shinikizo la mabadiliko ya tabianchi.

Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limesema El Niño hii ina uwezekano wa kuimarika zaidi katika kipindi chote cha mwaka 2026, jambo ambalo linaweza kusababisha ongezeko la hali mbaya ya hewa katika sehemu nyingi za dunia.

Utabiri kadhaa kutoka kwa mashirika ya kitaifa ya hali ya hewa unaonyesha kuwa huenda tukashuhudia moja ya El Niño kali zaidi kuwahi kurekodiwa, inayoweza kuitwa “super El Niño”.

Hata hivyo, wataalamu wanasema ni vigumu kubaini kwa usahihi muda na nguvu halisi ya El Niño, na kwa sasa wanafuatilia kwa karibu hali katika eneo maalumu la Bahari ya Pasifiki ya kati ambalo hutoa dalili za mabadiliko ya mfumo huo wa hali ya hewa.

No comments