CCM: TANZANIA HAIGAWANYIKI



CHAMA Cha Mapinduzi kimesema Tan zania haigawanyiki. Kimehimiza wananchi waendelee kulinda amani na utulivu uliopo kwa kukataa kila aina ya udini, ukabila au ukanda, kwani wakiyaruhusu yataligawa taifa. 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihon gosi amesema mambo hayo hayana nafasi na badala yake waunganishwe na Utanzania wao, utu wao na wapendane kwa kuangalia utaifa wao. 

Kihongosi alisema hayo akizungumza na wananchi katika eneo la Ayalagaya, Kata ya Dareda wilayani Babati mkoani Manyara jana. Alisema Tanzania haigawanyiki kwa kuwa imeendelea kuwa mfano wa utulivu kutokana na umoja na upendo wa wa nanchi wake. 

“Tanzania yetu haiga wanyiki, Mungu alivyo tupa nchi hii na kama ambavyo nyinyi watu wa Babati mmepewa ardhi hii kuwa makazi yenu basi mna wajibu wa kuilinda.Hapa ni nyumbani kwenu, msikubali mtu yeyote aje kucheza na utulivu wa maeneo yenu,” alisema Kihongosi. 

Alisema ni muhimu Watanzania waendelee kulinda umoja wa taifa na kupinga dhana ya ukabila, udini na ukanda.“Tukatae kwa sababu tutaigawa nchi hii, lazima tuunganishwe na Utanza nia wetu, utu wetu, hilo ndio jambo la msingi,” alisema Kihongosi. 

Akiwa katika ziara hiyo wilayani Babati alishiriki kikao katika Shina Namba Mbili kwenye Kata ya Bonga na akasisitiza wananchi wawe makini na wageni wanaowapokea ili kulinda usalama katika maeneo yao. 

“Mnapopokea wageni ni muhimu kuchukua tahad hari na kujiridhisha kuwa ni watu salama. Tusije tukawapokea watu wenye nia mbaya au wahalifu ambao wanaweza kuleta matatizo katika maeneo yetu,” alisema Kihongosi. 

Pia, alitembelea na ku kagua majengo ya huduma za dharura na wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Man yara yaliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 1.6.

No comments