SIMBU AING’ARA TENA BOSTON, AIBUKA WA PILI NA KUVUNJA REKODI MPYA YA TAIFA
Mwanariadha Sajinitaji Alphonce Felix Simbu, ameendelea kuandika historia katika riadha ya kimataifa baada ya kushika nafasi ya pili kwa mwaka wa pili mfululizo kwenye mashindano makubwa ya Boston Marathon, yaliyofanyika leo Jumatatu Aprili 20, 2026, huko Boston, nchini Marekani.
Aidha Simbu amekimbia kwa muda wa 2:02:47, muda ambao ni rekodi mpya ya kibinafsi na rekodi mpya ya Kitaifa kwa Tanzania.
Hii inakuwa mara ya pili mfululizo kwake kuibuka wa pili katika mbio hizo, jambo linaloendelea kuthibitisha hadhi yake kama mmoja wa wakimbiaji bora barani Afrika na duniani.
Post a Comment