RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA IKULU YA TUNGUU, ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo rasmi na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Chen Mingjian, katika Ikulu ya Tunguu, Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika tarehe 28 Julai, 2026, Rais Dkt. Samia amepokea salamu maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping, zilizowasilishwa kwake na Balozi huyo.
Viongozi hao wawili walitumia fursa hiyo kujadili masuala mbalimbali ya kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na China.

Post a Comment