Michael Oliver: Mwamba Anayezikwepa Newcastle na Sunderland! ⚽🔥
Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) haina baridi, na mwamuzi maarufu Michael Oliver amezidi kuingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuiongoza vyema mechi ya Man United dhidi ya Spurs iliyoisha kwa United kushinda 2-0.
Licha ya kuonekana kuwa "ndio mzee" uwanjani, Oliver ana kanuni zake kali zinazomfanya awe mbali na timu mbili mahususi.
Kwanini Oliver Hazigusi Timu Hizi? 🚫
Michael Oliver (40) ameweka wazi kuwa yeye ni shabiki lialia wa Newcastle United. Kutokana na sheria za kuepuka upendeleo (conflict of interest), haruhusiwi kabisa kuchezesha mechi inayowahusu 'The Magpies'.
Lakini si Newcastle pekee, pia amepigwa marufuku kuchezesha mechi za mahasimu wao wakubwa, Sunderland, ambao wamerudi EPL msimu huu. Oliver anasema hata kama mechi haihusu timu hizo lakini matokeo yake yana athari ya moja kwa moja kwa Newcastle (kama vile kuwania nafasi za Ulaya au kuepuka kushuka daraja), basi yeye anakaa kando ili kuepusha "shari".
Cristian Romero: Kadi Nyekundu Iliyomgharimu Zaidi! 🟥
Kwenye dabi hiyo ya hivi karibuni, Oliver hakupepesa macho pale alipomtoa nje beki wa Spurs, Cristian Romero, kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea rafu mbaya Casemiro.
Habari mbaya kwa mashabiki wa Spurs ni kwamba Romero hatokosa mechi tatu kama ilivyozoeleka, bali atakuwa nje kwa mechi nne mfululizo za ndani. Beki huyo mbishi atatarajiwa kurudi uwanjani kuanzia tarehe 15 Machi, jambo linalozidi kuongeza presha kwa kocha Thomas Frank.
Nini Kinafuata? 🏟️
Baada ya kazi safi Old Trafford, Oliver anatarajiwa kurudi kazini katikati ya wiki hii kwenye mzunguko wa 26 wa EPL. Ratiba itakuwa moto:
Chelsea vs Leeds
Man United vs West Ham
Man City vs Fulham
Vinara Arsenal vs Brentford
Post a Comment