SAMIA: Demokrasia Haipimwi kwa Ushindi, Bali kwa Maisha Baada ya Uchaguzi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan, amegusa mioyo ya Watanzania kwa
kusisitiza falsafa ya Umoja wa Kitaifa,
maridhiano, na kuheshimu kila sauti
Akizungumza mbele ya viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, baada ya kuapishwa jana Rais Samia alieleza bayana kuwa: “Demokrasia haipimwi kwa nani kashinda uchaguzi, bali kwa jinsi tunavyoendesha mambo yetu baada ya uchaguzi.”
Rais
Samia alitumia jukwaa hili kuwashukuru wagombea wengine 17 waliowania nafasi ya
Urais
Akisisitiza
umuhimu wa mazungumzo, Rais alionya wale wote waliochochea uvunjifu wa amani,
akisema: "Vurugu na uvunjifu wa amani huishia kupimana nguvu... ila mazungumzo huzaa mshikamano."
Akirejea
falsafa ya 4R's (Reconciliation,
Resilience, Reforms, Re Construction/Building)
Alibainisha
kuwa utekelezaji wa kina wa dhana ya Kazi
na Utu na mwelekeo wa Serikali kwa miaka mitano ijayo utatolewa rasmi
katika Hotuba ya Uzinduzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Aidha
Rais alizishukuru Jumuiya za Kimataifa na Kikanda, ikiwemo SADC, AU, na EAC,
kwa kuleta waangalizi

Post a Comment