RAIS SAMIA AKERWA NA VURUGU, ATOA AGIZO KWA VYOMBO VYA ULINZI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelaani vikali matukio
ya uvunjifu wa amani yaliyotokea katika baadhi ya miji nchini, huku akitaja
madhara mabaya ya vitendo hivyo na kutoa onyo kali kwa wachochezi.
Katika hotuba
yake ya kuapishwa, Mhe. Rais alieleza kusikitishwa na kuhuzunishwa na matukio
ya uvunjifu wa amani, akibainisha athari zake:
Rais
Samia alifafanua kwamba matukio hayo hayakwenda sambamba na taswira na sifa za Tanzania
Alitoa
onyo kwa wale wote waliochochea uvunjifu wa amani, akitaka watambue kuwa vurugu
huishia kupimana nguvu, ila mazungumzo
huzaa mshikamano
"Niwasihi
Watanzania tuchague hekima badala ya
ghadhabu; amani badala ya vurugu...
Usalama wa Taifa lolote hulindwa na wote kwa nguvu na gharama zozote"
Kama
hatua ya haraka, Rais Samia alitoa maagizo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,kuendelea
kufuatilia na kuchunguza kwa undani zaidi kilichotokea, huku akitaka nchi irudi
katika hali yake ya kawaida kwa haraka
Zaidi
ya hayo, Kamati ya Ulinzi ya Kitaifa, pamoja na Kamati za Ulinzi za Mikoa na
Wilaya, zimeagizwa kuhakikisha kwamba maisha
ya Wananchi yanarejea mara moja kuanzia leo
Mhe.
Rais alishukuru wagombea wengine 17 wa nafasi ya Urais
kwa kuonesha ukomavu wa kidemokrasia kwa kushindana kwa hoja, na kudhihirisha
kuwa siasa sio vita
Alikumbusha
kwamba, kwa mujibu wa falsafa ya 4R's, lengo la Serikali ni kuunganisha Taifa
kupitia kuzungumza na kuelewana
(Reconciliation)
Mhe.
Rais ameeleza kuwa masuala ya kina kuhusu mwelekeo wa
kazi za Serikali kwa kipindi kijacho, na ufafanuzi wa dhana ya Kazi na Utu,
utatolewa katika Hotuba ya Uzinduzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania

Post a Comment