Rais Samia kukutana na vyama vya siasa kupokea Ilani
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa atakutana
na vyama vingine vya siasa na kupokea ilanmi zao kwa moyo mkunjufu.,
Alisema hayo katika
hotuba yake baada ya kuapishwa mjini Dodoma jana.
Alisema kwamba ujenzi
wa Taifa unategemea ushirikishwaji wa wadau wote, baada ya kumalizika kwa msimu
wa uchaguzi.
Akishukuru wagombea
wengine 17 wa nafasi ya Urais kwa kuonesha ukomavu wa kidemokrasia, Mhe. Rais
alisisitiza kuwa mazungumzo huzaa
mshikamano,akitaja falsafa ya Serikali yake ya Awamu ya Sita ya 4R's ambayo inaanza na Reconciliation (kuzungumza na
kuelewana) na Resilience
(kuvumiliana).
Mhe. Rais alisema kila sauti inathaminiwa na kusisitiza
umuhimu wa ushirikishwaji. "Tutakuwa na nguvu zaidi pale kila sauti, chanya na hasi, zinaposikilizwa.
kuheshimiwa na kuthaminiwa..."
Kauli hii inaweka
wazi nia ya Serikali yake kupokea na kuzingatia mawazo na mapendekezo
yanayotolewa na pande zote, ikiwemo yale yaliyokuwa yameainishwa katika ilani
za vyama vingine vya siasa.
Wajibu wa Pamoja:
Dkt. Samia aliwaeleza
Watanzania kuwa demokrasia haipimwi na nani kashinda, bali kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa baada ya uchaguzi.
Aliongeza kuwa jukumu la kuponya penye maumivu na kujenga mshikamano si la
Serikali peke yake, bali ni kwa kila Chama
cha Siasa, Jumuiya za Wananchi, na kila mwananchi.
.jpeg)
Post a Comment