WAZIRI wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewataka wajumbe
wa baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuhakikishe vyama vya michezo vinaheshimu katiba
zao kwa kuheshimu vipindi vya uongozi na kufanya uchaguzi muda unapofika.
Dk.
Mwakyembe aliyasema hayo jana wakati akizindua baraza la 14 ambalo lilitangazwa
Februari 9, 2018 ambalo linaongozwa na Mwenyekiti Leodgar Tenga likiwa na
wajumbe sita pamoja na wajumbe wengine watatu ambao wanaingia kutokana na vyeo
vyao serikalini.
“Mwenyekiti napenda
kukupongeza wewe binafsi pamoja na wajumbe wote mlioteuliwa kuunda baraza la
14, vilevile ninampongeza kwa dhati
mwenyekiti na wajumbe wote waliokuwa katika baraza la kumi na tatu,” alisema.
“Tumefanya uteuzi wa wajumbe kwa kuzingatia
umakini na uwezo wenu kwa kila mmoja tukiwa na malengo ya kuongeza ufanisi wa
chombo hiki muhimu katika usimamizi wa maendeleo ya michezo nchini hivyo mmeteuliwa
ili kuleta mabadiliko katika Sekta ya maendeleo ya michezo,” aliongeza Dk.
Mwakyembe.
Alisema
baraza lihakikishe kuwa vyama vya michezo vinaheshimu katiba zao ikiwa ni
pamoja na kufanya uchaguzi kwa muda kwa kufuata kanuni za vyama husika muda
unapofika pia kuhakikishe viongozi hawabinafsishi na kuwavunja moyo wanachama
wao.
Baraza hilo
ambalo limeteuliwa na Waziri Dk Mwakyembe chini ya sheria ya BMT ya mwaka 1967
linaundwa na Leodgar Tenga ambaye ni Mwenyekiti.
Wajumbe ni
Profesa Mkumbwa Mtambo, Beatrice Singano, Kanali Mstaaafu Juma Ikangaa, John
Ndumbaro, Rehema Madenge na Salmin Kaniki.
Wengine
ambao wameingia kwa nafsi za vyeo vyao ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Yusuph Singo, Kamishna wa
Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Dk. Edicome
Shirima na Katibu wa BMT, Mohamed Kiganja.
No comments:
Post a Comment