SIMBA imerejea kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga
Ndanda FC mabao 2-0 katika mchezo
uliochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Alikuwa ni mshambuliaji John Bocco aliyepeleka kilio kwa Ndanda FC iliyokuwa inacheza mbele ya mashabiki wake baada ya kufunga mabao yote mawili katika kipindi cha pili baada ya dakika 45 kumalizika kwa suluhu

Bao la
kwanza alilifungwa dakika ya 52 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona
iliyopigwa na Shiza Kichuya na bao la pili lilifungwa dakika 56 akitumia
makosa ya mabeki wa Ndanda na kipa wao, Jeremiah Kisubi kuzembea kuokoa mpira
mrefu ulioingizwa kwenye eneo la hatari.
Ndanda walijitahidi kupeleka mashambulizi kwenye uwanja wa Simba,
wakiongozwa na mkongwe Mrisho Khalfan Ngassa, lakini umaliziaji mbovu
ukawakosesha kupata bao la kufuta machozi.
Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 12,
sawa na Azam FC walio nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao.
Yanga wenye pointi 21
ambao leo wanashuka dimbani wataendelea kushika nafasi ya tatu endapo
watashinda dhidi ya Mbao FC kama watatoa sare au kupoteza na Singida United
washinde dhidi ya Njombe Mji FC watashuka hadi nafasi ya nne.
Katika Uwanja wa Samora Iringa, Tanzania Prisons waliifunga Lipuli FC bao 1-0 lililofungwa na Salum Kimenya na Mtibwa Sugar iliifunga Majimaji mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Manundu Turiani, Morogoro.

Kikosi cha Ndanda FC kilikuwa, Jeremiah Kisubi, William
Lucian, Abdallah Suleiman/Ayoub Masoud dakika 51, Ibrahim Job, Hamad Waziri,
Hemed Khoja/Omar Mponda dakika 61, Jacob Massawe, Majid Khamis, John Tibar/Alex
Sethi dakika 72, Jabir Aziz na Mrisho Ngassa.
Kikosi cha Simba ni Aishi Manula, Paul Bukaba, Shiza Kichuya, Juuko Murshid, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, John Bocco, James Kotei/Yussuf Mlipili dakika 72, Juma Luizio/Moses Kitandu dakika 54, Muzamil Yassin na Mohamed Ibrahim ‘Mo’/Said Ndemla dakika 38.

No comments:
Post a Comment