OBREY Chirwa leo amezidi kudhirisha ubora wake Yanga akiifungia mabao matatu ‘hat trick’ ilipoibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Mbeya
City katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Tangu mwanzo wa
mchezo, Chirwa alionekana kuisumbua ngome ya City ambapo alikuwa akiwachomoka
mabeki wa timu hiyo mara kwa mara.
Chirwa alianza kuing’arisha
Yanga katika dakika ya 28 kabla Emmanuel Martin hajafunga bao la pili dakika
tatu baadae akitumia vizuri uzembe wa kipa wa City, Fikirini Bakari.
Dakika moja baada ya
kuanza kwa kipindi cha pili, Chirwa aliifungia Yanga bao la tatu kwa mkwaju wa
penalti iliyotolewa na mwamuzi Athumani Lazi wa Morogoro baada ya Raphael Daudi
kuchezewa rafu na kipa wa City, Fikirini akiwa anaelekea kufunga.
Chirwa ambaye ni
mchezaji bora wa Oktoba, alifunga bao lake la tatu, likiwa la nne kwa timu yake
katika dakika ya 59 baada ya kuunganisha pasi ya Daudi.
Hat trick ya Chirwa
ni ya pili kwenye Ligi Kuu msimu huu, ya kwanza ilikuwa ya Emmanuel Okwi wa
Simba aliyofunga kwenye mechi ya ufunguzi ya ligi dhidi ya Ruvu Shooting ambapo
Simba ilishinda mabao 7-0.
Karamu ya mabao
ilihitimishwa katika dakika ya 88 kupitia kwa Emmanuel Martin akiunganisha pasi
ya Gadiel Michael na kuujaza mpira wavuni.
Matokeo hayo yanaibakisha
Yanga bafasi ileile ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 20,
nyuma ya Azam yenye pointi 22 sawa na Simba inayoongoza msimamo kwa uwiano
mzuri wa mabao.
Azam ilicheza na
Njombe Mji ugenini Njombe na kushinda bao 1-0 huku Kagera Sugar nayo ikitamba
ugenini kwa ndugu zake Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Manungu, Turiani kwa
ushindi wa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment