LIGI Kuu
England imezidi kushika kasi, baada ya michezo ya jana kushuhudia miamba
Arsenal, Liverpool, Chelsea na Manchester City ikipata ushindi katika michezo
yao.
Arsenal
iliifunga Tottenham mabao 2-0 Uwanja wa Emirates, matokeo yaliyoifanya ifikishe
pointi 22 ikiwa ni moja nyuma ya Tottenham yenye pointi 23, lakini ikibaki nafasi
yake ya sita pamoja na ushindi huo.
Ushindi huo
wa Arsenal dhidi ya Spurs ni kama unahitimisha ubishi baina ya wapinzani hao wa
mji mmoja kuwa ni nani mbabe wa London.
Shokdran
Mustafi alikuwa wa kwanza kuiandikia Arsenal bao kwa kichwa dakika a 36,
akiunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo Mesut Ozil baada ya
Alexis Sanchez kufanyiwa madhambi.
Kisha Alexis
Sanchez alipigilia msumali wa moto jeneza la Spurs kwa kuifungia Arsenal bao la
pili dakika ya 41 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Alexander Lacazette.
Katika mechi
hiyo Arsenal ilifanya mabadiliko mawili katika kikosi kilichofungwa mabao 3-1 na
Manchester City.
Ilimuanzisha
Alexander Lacazette, lakini pia beki Shokdran Mustafi akirejea kutoka majeruhi
akicheza badala ya Francis Coquelin, ambaye hata hivyo aliingia kipindi cha
pili.
Nayo Spurs
ilifanya mabadiliko ya wachezaji watano kwenye timu iliyoibuka na ushindi dhidi
ya Crystal Palace, ikiwakaribisha kipa Hugo Lloris, Kieran Trippier, Ben
Davies, Dele Alli na Moussa Dembele na Harry Kane.
Katika mechi
nyingine Manchester City iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leicester na
kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa na pointi 34.
Mabao ya
City yalifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Gabriel Jesus dakika ya
45 na lingine likifungwa na kiungo wa kimataifa wa Ubeligiji, Kevin de Bruyne
dakika ya 49.
Chelsea nayo
ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya West Browich. Mabao ya Chelsea yalifungwa
na Alvaro Morata dakika ya 17, Eden Hazard dakika ya 23 na 62 na Marcos Alonso
dakika 38.
Nayo
Liverpool ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Southmpton.
No comments:
Post a Comment