WACHEZAJI
watano wa timu ya Taifa ya Mpira wa Meza wamekwenda nchini China kuweka kambi
kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa
kufanyika nchini Australia, mwakani.
Akizungumza
jana Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Meza (TTA) Issa Mtalaso alisema
wachezaji waliondoka ni watano kati yao wawili ni wanaume.
“Tumepata
bahati wachezaji wetu wamepata kambi ya siku 80 nchini China na wanaondoka leo
(jana) naamini kambi hii itakuwa chachu ya kufanya vizuri katika mashindano ya
Australia,” alisema Mtalaso.
Mtalaso
aliwataja wachezaji hao waliondoka kuwa ni Fathiya Hassan, Masoud Mtalaso, Amon
Amaniel, Mwanvita Mohamed na Neema Mwaisuila na kocha Ramadhan Othuman
ataungana nao baadae kwasababu bado hajapata kibali cha kutoka nje ya nchi.
Naye Katibu
Mkuu wa Kamati ya Olyimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi alisema anaishukuru
serikali ya China kwa kuwapa kambi hiyo ambayo pia wamegharamia tiketi za
kwenda na kurudi na wataalamu wa kuwafundisha.
“China
inafanya vizuri katika Mpira wa Meza hivyo kambi hii itawasaidia wachezaji wetu
katika mbinu hivyo naishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa kwa kuwapatia kambi hiyo,” alisema Bayi
Pia Bayi
alisema anatarajia timu ya ngumi za ridhaa itapata kambi nchini Cuba na riadha
itapata kambi nchini Ethiopia kwani bado wizara ya michezo inaendelea
kuwasiliana na balozi za nchi hizo hapa nchini kupitia kitengo cha diplomasia
ya michezo.
No comments:
Post a Comment