KIUNGO mshambuliaji
wa JKT Ruvu, Rashid Chambo amefuzu majaribio katika timu ya AFC ya Sweden.
Akizungumza
baba mzazi wa Rashidi mzee Mohamed Chambo ambaye ndiye meneja wa mwanae alisema
amefurahi kuona mwanae anakwenda kucheza soka la kulipwa.
“Rashid ni
mchezaji mwenye kipaji cha soka kuanzia akisoma nchini Uganda hivyo kufuzu
kucheza soka la kulipwa anatimiza ndoto yake ambayo amekuwa nayo,” alisema
Chambo.
Pia Chambo
alisema Rashid anatarajiwa kurejea nchini Novemba 27 na mwakani Januari 7
atarudi Sweeden kuanza maisha ya kucheza soka la kulipwa.
Kinda huyo
mwenye miaka 17 ambaye alikuwa anacheza Serengeti Boys iliyofuzu AFCON za Gabon
atakuwa anacheza timu ya vijana lakini pia kocha wa AFC ameshauri awe anacheza
kikosi cha wakubwa.
AFC ndiyo
timu anayofanya majaribio Said Hamis Ndemla pia anacheza Thomas Ulimwengu
No comments:
Post a Comment