TANZANIA
imeng’ara katika soka la ufukweni baada ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) kuitangaza ni ya 12 katika viwango vya mchezo huo katika Bara la
Afrika.
Akizungumza
Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limetoa viwango hivyo na Tanzania
inashika nafasi ya 86 duniani na Afrika 12.
“Tanzania
imeng’ara kwa mujibu wa viwango vilivyotangazwa juzi nchi za Senegal, Nigeria,
Misri, Morocco, Madagascar, Ivory Coast, Ghana, Libya, Msumbiji, Cape Verde na
Kenya ndizo zilizo juu ya Tanzania,” alisema Lucas.
Taarifa
imekuja huku Tanzania ikiwa bado haijawahi kuwa na ligi ya mchezo huo zaidi ya ligi
inayohusisha timu za taasisi za Elimu ya juu mkoa wa Dar es Salaam na Pwani
pekee inayotarajiwa kuanza Novemba 9 katika Uwanja wa Karume Dar es
Salaam.
Mbali na
ligi hiyo ya soka la ufukweni Tanzania imeshiriki mashindano ya kimataifa ya
Afrika mara mbili, ambayo ndio imeipaisha katika viwango hivyo vya ubora.
No comments:
Post a Comment