KAMATI ya
nidhamu na rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemwachia huru Wakili
Dk. Damas Ndumbaro na aliyekuwa kocha msaidizi wa Geita Gold Mining Choki Abeid
na kutupa rufaa nyingine tatu.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana Mwenyekiti wa kamati hiyo Rahimu Shaban alisema
kamati yake ilikutana Jumapili kujadili warufani watano ambao ni Damas
Ndumbaro, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Tabora Yusuph Kitumbo na
wenzake waliofungiwa maisha kujihusisha na soka.
“Tuliketi
kusikiliza rufaa ya Damas Ndumbaro, Yusuph Kitumbo, Fechi Remtullah, Thomas
Mwita na Choki Abeid na niwaeleze tu kwa kifupi kamati imemwachia huru Damas
Ndumbaro baada ya kupitia vielelezo alivyowasilisha mbele ya kamati,”.
“Baada ya
kamati kukaa na kupitia kwa kina maelezo ya Ndumbaro kamati ilijiridhisha
kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi kati yake na Mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili
Jerome Msemwa na pia hakupewa nafasi ya kusikilizwa japo alitoa udhuru kabla ya
shauri kusilizwa,”
Ndumbaro
aliwasilisha barua ya kujitoa kwenye kesi iliyokuwa inamhusu Rais wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi hivyo kamati ilijiridhisha uwepo wa
mgongano wa kimaslahi na pia hukumu iliyotolewa ilitolewa kwa wingi wa kura.
“Hukumu
inasema imetolewa kwa wingi wa kura ambazo ni kura tatu za ndio dhidi ya moja
ya hapana lakini haielezi kwenye akidi nani alikuwepo kwenye kikao hicho hivyo
inatosha kueleza pasi na shaka kuwa akidi haikutimia,” alisema Shaban.
Aidha Shaban
alisema kamati imeona ni busara kumwondolea kifungo hicho ambacho ameshatumikia
kwa miaka miwili na miezi tisa toka afungiwe
Naye Choki
Abeid aliyekuwa kocha msaidizi wa Geita Gold Mining amefunguliwa kutoka kifungo
cha maisha kwasababu kosa lake haliendani na hukumu aliyopewa kwani alikuwa
anatimiza majukumu yake.
“Kazi ya
kocha ni kufundisha ili mchezaji acheze na soka ni mchezo wa kiungwana hivyo
kocha kumsihi mchezaji kurudi uwanjani ili acheze ni moja ya majukumu yake,”
alisema Shaban.
Kuhusu
Yusuph Kitumbo, Fechi Remtullah na Thomas Mwita ambao walihikumiwa kifungo cha
maisha kwa kujihusisha na kupanga matokeo ya mchezo wa Ligi daraja rufaa zao
zimetupwa.
Awali
Ndumbaro alifungiwa miaka saba na Kamati ya Nidhamu kutojihusisha na soka
wakati akitetea klabu kuhusu maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya TFF kukata fedha
za udhamini wa klabu na mapato ya milangoni.
Ndumbaro
alikuwa wakili wa klabu za ligi kuu hivyo ulikuwa wajibu wake kutetea wateja
wake kukatwa asilimia tano ya fedha za udhamini na Sh. 500 ya kila tiketi
inayokatwa na shabiki kuingia uwanjani.
Katika madai
hayo Ndumbaro alidai kuwa Kanuni za Ligi zilizopitishwa kutumika kwa ajili
msimu huu, hususan kuhusu makato ya fedha za milangoni si sahihi kwa vile
zimerekebishwa na Kamati ya Mashindano ya TFF badala ya Kamati ya Sheria na
Hadhi za Wachezaji ya shirikisho
Kamati hiyo
ilimfungia Ndumbaro kwa kuzingatia Ibara ya 41(6) cha Kanuni za Ligi za TFF
toleo la 2014 kujihusha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha
miezi 12.
Na Ibara 41(16) cha Kanuni za Ligi za TFF
toleo la 2014 kamati ilimfungia kutojihusisha na shughuli za soka ndani na nje
ya nchi kwa miaka saba, hukumu iliyotolewa Oktoba 13, 2014.
Ndumbaro alikuwa mtu wa kwanza kufukuzwa uanachama wa TFF tangu Kamati mpya wa Utendaji ya shirikisho hilo chini ya Rais Jamal Malinzi iingie madarakani.
Ndumbaro alikuwa mtu wa kwanza kufukuzwa uanachama wa TFF tangu Kamati mpya wa Utendaji ya shirikisho hilo chini ya Rais Jamal Malinzi iingie madarakani.
No comments:
Post a Comment