TIMU ya soka ya
Taifa Stars inashuka dimbani leo Jijini Kigali, Rwanda kuwania kufuzu kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) dhidi ya
Rwanda, Amavubi.
Taifa Stars
inajitupa uwanjani ikiwa imeongezewa nguvu na mshambuliaji wa Yanga, Simon
Msuva aliyeachwa wakati Stars ilipoondoka Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa marudiano baada ya timu hizo
kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Jumaosi iliyopita Uwanja
wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo wa leo ni
muhimu kwa Stars kwani inahitaji ushindi au sare ya mabao 2-2 isonge mbele na
kucheza ama na Uganda au Sudan Kusini ambazo zinarudiana pia.
Katika mchezo wa
awali uliofanyika Sudan Kusini, zilitoka suluhu. Sare ya 1-1 inaiweka Taifa
Stars katika wakati mgumu kwani zikitoka suluhu leo au kufungana au ikafungwa,
itatolewa.
Kocha Mkuu wa
Taifa Stars, Salum Mayanga anatakiwa kupanga kikosi imara ambacho kitacheza kwa
bidii na kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo.
Msuva aliyebaki
kushughulikia mipango ya kujiunga na timu moja ya Morocco, anatarajiwa
kuiongezea Stars nguvu na hivyo kutoa matumaini ya ushindi.
Hata hivyo, Taifa
Stars inatakiwa kuacha ndoto za kutoka sare kwani kufanya hivyo kutaikosesha
nafasi ya kuelekea kufuzu kwa mara ya pili kwa fainali hizo baada ya kucheza
kwa mara ya kwanza mwaka 2009 Ivory Coast.
Katika fainali
hizo, Tanzania ilipangwa Kundi A na Senegal, wenyeji Ivory Coast, Zambia na
Senegal. Ilimaliza ikiwa ya tatu kwa kuwa na pointi nne.
Zambia na Senegal
zilifuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya kumaliza nafasi ya kwanza na pili
kila moja ikiwa na pointi tano zikitofautiana mabao.
Katika kikosi cha
sasa cha Stars, ni Erasto Nyoni pekee alikuwemo katika kile kilichocheza fainali
hizo mwaka 2009 ambacho kilishinda 1-0 dhidi ya Ivory Coast, kilifungwa 1-0 na
Senegal na kutoka sare ya 1-1 na Zambia.
Baada ya mchezo
wa Mwanza, Stars ilitua mapema Kigali, Rwanda kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa
ili iweze kupata matokeo mazuri katika mchezo wa leo.
Bado Taifa Stars
ina kazi ngumu kwani kikosi hicho hakijaelewana vizuri na Rwanda sio timu ya
kubeza kwani wako vizuri na wanacheza kwa kuelewana.
Kocha Mayanga
alisema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo na kitapambana `kiume’ kuibuka na ushindi katika mchezo utakaopigwa
Uwanja wa Amahoro.
Naye nahodha wa
timu hiyo, Himid Mao alikaririwa akisema kuwa atahakikisha timu yake inacheza
vizuri kushinda.
Waamuzi wa mchezo
Mchezo
utachezeshwa na Brian Nsubuga Miiro huku akisaidiwa na Ronald Katenya na Dick
Okello. Wa akiba ni Chelanget Ali Sabila. Kamishna wa mchezo atakuwa Ali
Mohamed Ahmed kutoka Somalia.
WAGANDA KUCHEZESHA
MECHI YA STARS NA RWANDA LEO
A+
A-
Print
Email
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Afrika (CAF), limewateua waamuzi wa Uganda
kuchezesha mchezo wa marudiano kati ya timu ya taifa ya Rwanda “Amavubi”
na Taifa Stars ya Tanzania kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani (CHAN).
Stars na Rwanda zinarudiana leo Jumamosi kwenye uwanja wa Nyamilambo
mjini Kigali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 jijini Mwanza wiki
iliyopita na timu inayoshinda ndio itakayofanikiwa kusonga mbele.
Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua utachezwa saa 10:00
jioni kwa saa za Rwanda ambazo ni sawa na 9:00 alasiri kwa saa za
Tanzania na utachezeshwa na Brian Nsubuga Miilo ambaye ni raia wa Uganda
atakayepuliza kipyenga cha kati.
Atasaidiana na Ronald Katenya (Line 1), pamoja na Dick Okello (Line 2),
wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Cheleneti Ally Sabila hukukamishina wa
mchezo atakuwa ni Ally Ahmed Mohammed kutoka Somalia.
Stars ina matumaini ya kusonga mbele kutokana na rekodi yake ambapo hadi
sasa imecheza jumla ya mechi 10 za kimataifa, imeshinda mechi nne, sare
tano na kupoteza mchezo mmoja wa nusu fainali ya michuano ya COSAFA.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2017/07/waganda-kuchezesha-mechi-ya-stars-na.html#more
Copyright © saluti5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2017/07/waganda-kuchezesha-mechi-ya-stars-na.html#more
Copyright © saluti5
No comments:
Post a Comment