Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeshindwa kufurukuta kwenye uwanja wake wa nyumbani, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wageni wao Rwanda, 'Amavubi'.
Mchezo huo wa kuwania kufuzu fainali zijazo za mataifa ya
Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani, ulishuhudia Stars
ikicheza mbele ya Watanzania lukuki ikishindwa kupata ushindi.
Rwanda, Amavubi ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa
Dominique Nshuti kunako dakika ya 17 kipindi cha kwanza, mlinzi Shomari
Kapombe aliumia baada ya kuchezewa rafu mbaya na kutolewa nje.
Stars ilisawazisha bao katika dakika ya 34 kipindi hicho
hicho cha kwanza kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na nahodha wake Himid
Mao Mkami 'Ninja' baada ya beki wa kushoto Gardiel Michael kuangushwa.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa sare, kipindi cha pili
kilianza kwa kasi na kila timu zilishambuliana kwa zamu lakini hadi
mwisho miamba hiyo ya Afrika mashariki ilimaliza kwa sare, kwa matokeo
hayo, Stars imejiweka shakani kutinga hatua inayofuata kwani inahitaji
sare ya kufungana zaidi ya bao moja ama kushinda wakati Rwanda inahitaji
sare tasa tu ili kusonga mbele
No comments:
Post a Comment