SERIKALI imeipongeza
Taasisi ya Tulia Trust kwa kufadhili vijana 20 kutoka Tukuyu, Mbeya elimu ya
sanaa katika Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TaSUBa)
Akizungumza
katika hafla ya kufunga mafunzo maalum ya miezi miwili jana, Kaimu Mkurugenzi wa
Utamaduni, Leah Kihimbi aliwashukuru vijana hao kwa kukubali kupokea mafunzo
hayo.
Kihimbi
aliwataka vijana hao kutumia mafunzo hayo kuchochea jamii kupenda utamaduni
wetu na kurejea katika misingi ya vyakula, mavazi na sanaa.
“Naamini
hamtofanya sanaa Mbeya pekee bali mtapanua wigo katika mikoa mingine hivyo mtakuwa
mabalozi wa ngoma za asili hapa nchini,” alisema Kihimbi
Aidha aliwaasa
vijana hao wakatumie ujuzi walioupata Bagamoyo kwa wenzao wa Mbeya na kuongeza
kuwa mafunzo hayo wayafikishe kwa wanawake ambao hawakushiriki mafunzo.
Naye Kaimu
Mtendaji wa TaSUBa, Gabriel Kiiza alisema mafunzo ya vijana hao yaliyoanza
Aprili 18-Juni 16 kwa ushirikiano TaSUBa
na Tulia Trust na kuwaomba wadau wengine kuiga mfano wa Tulia Trust
“Tunaipongeza Tulia Trust kwa kuwaendeleza
vijana ambao walikuwa hawana elimu ya sanaa, hivi sasa watafanya kazi yao kwa
weledi zaidi tofauti na ilivyokuwa awali,” alisema Kiiza.
Balozi wa
Tulia Trust, Hassan Ngoma alisema vijana 20 waliopata mafunzo Bagamoyo ni zao
la Maonesho ya Utamaduni Tulia yaliyofanyika mwaka jana wilayani Tukuyu, hivyo
shindano la mwaka huu wanatarajia kuongeza ushindani kwa vijana watakaoshiriki
maonesho yanayotarajia kuanza Septemba 21-23.
Ngoma
alisema mbali ya kusaidia sanaa, pia Tulia Trust ni waandaaji wa Tulia Marathon
na vikundi vya uchumi kwa akina mama.
“Tumepanga kuendeleza ushirikiano utaendelea
kati yao na TaSUBa, wengine waige mfano huo ambao utasaidia sanaa yetu katika
anga la Kimataifa,” alisema Ngoma.
Katika hafla
hiyo, vijana hao walikabidhiwa vyeti huku wengine wanne kati yao wakichaguliwa
kuendelea na masomo ya cheti baada ya kufanya vizuri.
No comments:
Post a Comment