FOMU za
kuomba uongozi katika Chama cha Soka la Wanawake (TWFA) zinatarajiwa kuanza
kutolewa Juni 19 katika ofisi za Hosteli ya TFF, Karume na uchaguzi utafanyika
Julai 8.
Akizungumza
na wandishi wa habari juzi Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, George
Mushumba alisema nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu
Msaidizi fomu zitanunuliwa kwa Sh 200,000 wakati nafasi za Mweka Hazina, Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji fomu
zitapoatikana kwa Sh 100,000.
“Fomu za
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi zitaanza kutolewa Juni 19, mwaka huu na
kwamba mwisho wa kuchukua na kurudisha ni Juni 22, mwaka huu saa 10.00 jioni,”
alisema Mushumba.
Juni 23,
Kamati itapitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali na Juni
24 Kamati itatangaza majina ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za
uchaguzi kwa mujibu wa katiba au kanuni za TWFA.
Juni 26 na
27, itapokea pingamizi kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni na Juni 28
kamati itapitia pingamizi.
Juni 29
kamati itatoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau na Juni 30
NI usaili kwa wagombea waliotangazwa
Julai Mosi
kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa, Julai 02, kamati kupokea rufaa,
Julai 03 kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa
Julai 04
kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea, Julai 04 hadi 07 wagombea
kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili na
Julai 08 uchaguzi Mkuu wa TWFA
Mushumba
alisema nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu,
Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne
wa Kamati ya Utendaji na sifa ya elimu kwa wagombea wote ni kidato cha nne.
No comments:
Post a Comment