KAUZU
imemaliza vita ya majirani wa Temeke baada ya kuifunga Sheraton FC mabao 2-1
kwenye mchezo uliochezwa jana katika Uwanja wa Tandika Mabatini, Temeke
Timu hizi
majirani kama ilivyo Liverpool na Everton za England zina ushindani lakini Kauzu
walipata bao la kwanza dakika ya tano lililofungwa na Hamad Kibopile.
Kama
haitoshi dakika 23 Kauzu wakapata bao lao la pili lililofungwa na Awadh Said na
kwenda mapumziko Kauzu wakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha
pili Sheraton walicharuka na kufanikiwa kufunga bao dakika ya 56 ambalo lilidumu
hadi dakika 90.
Kauzu
wanaongoza Kundi H wakiwa na pointi tatu wakifuatiwa na Faru Jeuri na Miami
ambao wote wana pointi mojamoja huku Sheratoni wakiwa mkiani bila pointi.
Katika
mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Ilala Faru Jeuri walitoshana
nguvu na Miami baada ya kutoka suluhu.
No comments:
Post a Comment