Wednesday, June 21, 2017
MIRAJI ADAM ACHEKELEA MILIONI 20 ZA SINGIDA UNITED, ASAINI MIAKA MIWILI
BEKI wa African Lyon, Miraji Adam amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Singida United wenye thamani ya Sh 20 milioni ambazo amesema hajawahi kuzipata tangu aanze kucheza soka lake.
Usajili huo umefanyika leo Jumatano mchana jijini Dar es Salaam ambapo ametamka kwamba amefanya uamuzi huo kwani anaona Singida United ni sehemu sahihi kwake.
Akizungumza Miraji alisema kuwa miaka yote aliyocheza soka ikiwemo klabu kubwa hapa nchini ya Simba hakuwahi kupewa pesa nyingi kama hiyo zaidi aliishia kukamata Sh 15 milioni ambazo pia alipewa kwa awamu.
“Yaani hapa ni kama naanza kufaidi soka kwani sijawahi kusajiliwa kwa pesa kama hii, nilipewa pesa kidogo ambayo pia ilitolewa kwa mafungu ambapo kufanya jambo lako kwa wakati mmoja ilikuwa ni vigumu.
“Hapa nimelipwa pesa yote ambapo nitaweza kufanya jambo la maana kwa wakati mmoja, naahidi kwamba nitajituma zaidi kuisaidia timu kwani nao wanaonekana wamejipanga hivyo sitawaangusha,” alisema Miraji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment