SERIKALI ya
wilaya ya Ubungo imempa heshima kiungo mshambuliaji wa Tottenham ya England na
timu ya Taifa ya Kenya, Victor Wanyama kwa kuipa moja ya barabara za Ubungo
jina lake.
Wanyama
ambaye pia alikuwa mgeni wa heshima kwenye mchezo wa mashindano ya Ndondo kati
ya FC Kauzu dhidi ya Faru Jeuri baada ya kuzindua alifurahi kutambuliwa na
kupewa heshima nje ya nchi yake.
“Ni kitu kizuri kwangu ina maana kubwa kwa
sababu kutambuliwa nje ya nchi yako si rahisi sana, imenifundisha najua kila
mtu anaponiangalia apata motisha na mambo yote ninayofanya
yanaonekana, nawashukuru na nawaambia asante,” alisema Wanyama.
Naye Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jacob Boniface alisema zawadi walioamua kumpa
Wanyama itafanya wachezaji kutoka mataifa mengine kuja Tanzania kutokana na
wageni wanavyopokelewa.
“Sisi
tunashukuru kama manispaa ya Ubungo tumepata hamasa kubwa ya michezo ambayo
inafanyika kwenye maeneo ya Halmashauri ya manispaa ya Ubungo na halmashauri ni
mpya na watu wanavyofurika kuona nafarijika sana.”
“Tumefarijika
na ujio wa Wanyama mchezaji kutoka timu ya Tottenham ya England na halmashauri
ya Ubungo imempatia jina kwenye moja ya barabara zake ambazo zipo katika eneo
hili kwa hiyo wanamichezo wote watakaokuwa wanakuja watakuwa wanaona jina la
Victor Wanyama,” alisema Jacob
Baada ya kuzindua barabara hiyo Wanyama alikwenda kuangalia
mchezo kati ya Kauzu na Faru jeuri kwenye Uwanja wa Kinesi, Unbungo ambapo
Farujeuri ilishinda kwa bao 1-0.
Baada ya
kusalimiana na wachezaji alizungumza na wachezaji na kusema yeye amewahi kucheza ndondo
akiwa Kenya ambapo kwao wanaiita ‘Kothbiro’ ikiwa na maana ya msimu wa mvua.
“Kwetu pia
kuna ndondo sisi tunaiita ‘Kothbiro’ nikiwa na timu yangu ya mtaani inayoitwa
Ziwani na Kothbiro manaa yake ni msimu wa mvua, wanaocheza ni wachezaji wa
mitaani na wachezaji wanaocheza ligi kuu wanachanganyika pamoja,”
“Kothbiro
ina nafasi kubwa Kenya kwa sababu imetoa wachezaji wakubwa na inasaidia timu za
ligi kupata wachezaji kwa sababu makocha mbalimbali wa ligi huwa wanahudhuria
kuangalia vipaji,” alisema Wanyama.
Wanyama alisema
anatarajia kushuhudia mechi kali yenye ushindani kwa sababu ameambiwa timu hizo
zilishawahi kukutana kwenye fainali ya michuano hiyo.
Wanyama
azungumzia jezi namba 67
Victor
Wanyama alisema alivyosajiliwa Celtic ya Scotland alichagua kuvaa jezi namba 67
ambayo ni namba kubwa, lakini alifanya hivyo makusudi na haikuwa bahati mbaya.
Wanyama
alisema sababu kubwa iliyomfanya aache namba nyingine zote na kuchagua namba 67
ambayo kiuhalisia ipo mbali sana alisema alifanya uchunguzi na kugundua Celtic
ilishinda Champions League mwaka 1967.
“Kila
mchezaji ana ndoto, kwa hiyo nilivyokwenda pale nilikuwa na ndoto na nilikuwa
najua Celtic ni timu ambayo inashiriki Champions League hivyo nilikuwa na ndoto
siku moja niweze kushinda ubingwa wa Champions kitu ambacho bado sijafanikiwa
lakini bado nina ndoto.”
“Nilifanya
uchunguzi wangu nikagundua Celtic walishinda Champions League mwaka 1967 ndio
maana nikamua kuvaa namba 67 ili iwe kumbukumbu kwangu nikiingia ndani
nakumbuka mwaka wa mafanikio.”
Alipohamia
Southampton Wanyama amekuwa akivaa jezi namba 12 hadi sasa Totenham anavaa jezi
yenye namba 12 sambamba na akiwa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’.
Pia Wanyama
amezitaja sababu ambazo zinazosababisha wachezaji wa Afrika Mashariki kushindwa
kutoka kwenda kucheza nje ya Afrika kuwa ni kuridhika mapema na kukata tama
“Wachezaji wa huku tunakata tamaa mapema na
kuridhika haraka, kwa sababu unakuta mchezaji lengo lake ni kwenda kucheza Mali
akifika pale anatosheka badala kujituma ili afike mbali zaidi hata mimi kuna
wakati nilikaribia kukata tamaa lakini nilipambana kwa sababu nilikuwa nikijua
kuna wakati utafika mambo yatakaa sawa,”
“Kuchelewa
kuoneshwa kwa ligi zetu kumechangia wachezaji wengi wa ukanda wa Afrika
Mashariki kuchelewa kutoka kwenda nje ukilinganisha na mataifa mengine ya
Afrika hasa Afrika Magharibi,” alisema Wanyama.
Wanyama
alisema akiwa Ubelgiji kuna wakati mambo yalikuwa magumu kwa sababu alienda kule
kabla hajafikisha miaka 18 kwa hiyo hakuweza kucheza moja kwa moja bali
aliishia kufanya mazoezi akawa anawapigia simu nyumbani kutaka kurudi lakini
walimzuia kwa kuniambia kama ana nyumba arudi lakini kama hana aendelee kukaa
hukohuko.
Anasema
anamshukuru ndugu yake Mariga kwani alimshauri asirudi ndipo akaamua kupambana
akaendelea kukaa.
No comments:
Post a Comment