Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 17, 2016

SIMBA KUISHUSHA YANGA KILELENI KESHO


SIMBA na Azam FC kesho zinashuka dimbani kusaka pointi tatu kwenye viwanja tofauti katika michezo yao ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba itakuwa mgeni kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona  Mtwara dhidi ya Ndanda FC na Azam FC ikikaribishwa na African Lyon kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Wekundu hao wa Msimbazi huenda wakaendeleza rekodi yao ya kuifunga Ndanda FC  baada ya mchezo wao wa mzunguko wa kwanza kuwachapa mabao 3-1 katika mechi iliyochezwa Dar es Salaam.
Mchezo huo utakuwa wa kwanza katika ligi kwa kipa mpya wa Simba Mghana Daniel Agyei ambaye anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha kwanza  baada ya kipa Vicent Angban wa Ivory Coast kusitishiwa mkataba wake.
Pia, wachezaji wengine wapya ni kiungo James Kotei, mshambuliaji Pastory Athanas, Juma Luizio, Moses Kitandu na beki Vicent Costa.
Simba yenye pointi 35  inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kurejea kileleni mwa msimamo baada ya jana Yanga kuishusha. Yanga inaongoza kwa pointi 36 sasa.
Vile vile, Ndanda FC  yenye pointi 19 iliahidi kufuta rekodi ya kufungwa na timu hiyo ikijivunia kusajili wachezaji wawili wapya Ayub Shaban na Ismail Mussa watakaokuongeza nguvu.
Kwa upande wa Azam FC yenye pointi 25  itacheza leo kwenye uwanja wa Uhuru  ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Chamazi.
Pengine, mchezo wa leo Azam FC kwa vile imefanya mabadiliko makubwa ikafanya vizuri tofauti na African Lyon yenye pointi  17 ambayo imeondokewa na wachezaji wake wengi waliojiunga na Mbeya City.
Wachezaji wapya wanaotarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha Azam FC ni Samwel Afful, Mohamed Yahaya, Yakubu Mohamed, Enock Agyei, Stephani Kingue, Joseph Mahundi na Abdallah Kheri.
Azam FC inahitaji kushinda katika mchezo huo ili kuingia katika mbio za kuligombania taji la ligi.
Pia, Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya dhidi ya Majimaji huku Mbao FC ikiwa kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Mwanza ikiwakaribisha Stand United.

No comments:

Post a Comment