Na Rahel Pallangyo
WASHAMBULIAJI wawili raia wa Ghana, Yahaya Mohammed na Samuel Afful wamesajiliwa na klabu ya Azam FC, kwa ajili ya
kuichezea timu hiyo mzunguko wa pili.
Yahaya Mohammed ambaye alikuwa
anachezea timu ya Aduana Stars ameingia mkataba wa miaka miwili na Samuel Afful ambaye alikuwa anachezea
Sekondi Hassacan, amesaini mkataba wa miaka mitatu.
Mohammed ambaye anaongoza kwa
upachikaji wa mabao kwenye ligi ya kwao, mpaka sasa ana mabao 15 amesema
amefurahi kusajiliwa Azam FC, na kudai amekuja Azam kwa sababu ndio klabu
ilionesha nia ya kumwihitaji.
“Nimekuja Azam FC kwa sababu
walionesha nia ya kunihitaji na leo nimekuja kusaini mkataba nao, naamini
popote ukicheza kwa bidii unaweza kuonekana na kwenda mbele zaidi”, alisema
Mohammed.
Mohammed na Samuel wote wamecheza
timu za taifa za Ghana kwa nyakati tofauti kuanzia zile za U-20, U-23 na timu
kubwa (senior team)
Naye kocha wa Azam FC, Zeben
Hernandez amesema amefurahi kupata saini za wachezaji hao kwani itasaidia
kuziba pengo la wachezaji waliomaliza mikataba yao.
“Naamini mzunguko wa pili
tutaanza tukiwa na uhakika wa kufanya vizuri baada ya kuwapata wachezaji hawa”,
alisema Hernandez a,baye ameondoka jana usiku kwenda kwao kwa ajili ya
mapumziko mafupi.
No comments:
Post a Comment