CHAMA cha
wachezaji wa mpira wa miguu Tanzania (SPUTANZA) kimelitaka Shirikisho la soka
nchini (TFF) kupitia Kamati ya Utendaji kuweka kanuni za kila mchezaji
anayecheza ligi kuu, ligi daraja la kwanza na pili lazima awe mwanachama wa
chama hicho.
Mwenyekiti wa SPUTANZA, Mussa Kisoki amewaambia wandishi wa habari kuwa wachezaji wamekuwa wakisainishwa mikataba ambayo imekuwa ikiwabana na huwa wanakikumbuka chama hicho pale mambo yao yanapokuwa magumu.
Kisoki alisema dhamira yao ni kuishawishi Serikali kuwa soka la Tanzania liwe la kulipwa kwakuwa wachezaji wanalipwa pesa nyingi na itakuwa rahisi mchezaji kuhama kutoka timu moja kwenda nyingine kwa ajili ya maslahi kama ilivyo katika nchi zilizoendelea.
"Wachezaji wanasajiliwa hadi kwa Sh 20 milioni sasa kwanini isiwe rasmi soka la kulipwa na endapo itatambuliwa Serikali itakuwa vizuri kwakuwa maslahi ya wachezaji yatakuwa mazuri kuliko sasa," alisema Kisoki.
Akizungumzia suala la beki wa Yanga Hassani Kessy, Mwenyekiti huyo alisema mabingwa hao walivunja kanuni ya 69(5) ya ligi kwa kufanya mazungumzo na mchezaji bila kuwasiliana na Simba ambao ndiyo walikuwa wamiliki wa mchezaji huyo lakini Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF ndiyo walipaswa kulimaliza wenyewe suala hilo na sio kulitoa nje.
"Simba haina madai yoyote na Kessy ila wanawadai Yanga kwa kufanya mazungumzo na mchezaji bila kuwapata taarifa na ndiyo maana beki huyo anacheza ligi kwakua hana pingamizi," alisema Kisoki.

No comments:
Post a Comment